UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM)UNAUNDWA KWA MUJIBU WA KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI TOLEO LA MEI 2005 ( CCM) SEHEMU YA NNE, IBARA 129 (1) A
UTANGULIZI; Umoa wa vijana wa CCM ni chombo kinachowaunganisha vijana wake wa Tanzania wanao unga mkono sera , siaasa na itikadi ya ya chama cha mapinduzi. Shabaha za chama cha mapinduzi zakuunda umoja wa vijana kuwa shule ya kuandaa wanachama safi na viongozi bora wa CCM . kwa msabaha huo, Umoja wa vijana wa ccm Utaandaa vijana kuwa raia wema wa Taifa letu na kwamba chombo hiki nisawa na tanuri la chuma la kuhokea makada wazuri. Kwahiyo umoja wa vijana wa CCM ,unawajibu wa kuongeza shughuli zinazohusu maendeleo na maslahi ya vijana nchini, chini ya uongozi wa CCM na unakiri jukumu lake katika historia ya Taifa ya kuimarisha umoja wa kitaifa , kuendeleza mapinduzi ya kijamaa ya kidemokrasia na mapambano ya ukombozi katika Afrika, na duniani kote. Umoja wa Vijana wa CCM unatambua kuwa harakati za kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kujenga jamii iliyo sawa nchini Tanzania, Afrika na duniani kwa ujumla kunahitaji chombo madhubuti kinacho unganisha fikra na vitendo vy vijana wote , wakulima na wafanyakazi ,wanafunzi, vyama vya hiari, wafanya biashara na vijana wengine wa sekta za binafsi. Kabla ya umoja wa vijana wa ccm kuundwa , Vijana wa CCM wa Tanzania walikuwa katika malezi ya vyama vya vijana vya afro Shirazi Part (ASPYL) na Tanganyika African national Union (TYL), kabla yakuwa jumuiya ya wananchi katika chama cha mapinduzi. Umoja wa vijana wa CCM tunaounda , unakusudia kurithi yale yote mazuri ya ASPYL na TYL pamoja na itikadi ya vyama vya ASP na TANU na hasa kwa kutambua nafasi ya kihistoria ya vyama hivyo katika kumuondoa mwafrika kwenye unyonge, kunyanyaswa na kudharauliwa ili kufikisha kwenye uhuru wa kuheshimiwa. Umoja wa vijana wa CCM tunaounda , unakusudiwa uwe madhubuti katika muundo wake , na hasa kifikra na vitendo vya kufutilia mbali aina zote maki ya ukoloni mamboleo , ubeberu, unyonyaji, dhuruma, uonevu na unyanyasaji nchini . kwakuwa umoja wa vijana CCM unazingatia kwamba nguvu za vyama ndio lasilimali kuu ya Taifa letu na kukubali kimsingi dhana kwamba vijana ni viongozi wa Taifa la leo na kesho, tunataka umoja wa vijana wa ccm, uongoze harakati za kutetea maslahi ya vijana na uwe kiungo kati ya vijana wanamapinduzi wa Tanzania na wanamapinduzi wenzetu duniani kote na kuhakikisha kwamba chini ya uongozi wa CCM azma tuliyojiwekea ya ujamaa na kujitegemea tunaifikia
This Blog Powerd by:
Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 7350373432
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment